Publication

Kazi na wajibu wa Maafisa wa serikali waliochaguliwa

TYPE:
Ukweli wa kwamba wengi wa wananchi hawajui mipaka ya uchaguzi au kazi ya wale wanaowachagua kuchukua ofisiinaonyesha kwamba i) wapiga kura hawaambatanishi uchaguzi na upatikanaji wa haki kwa njia ya upokeaji wa huduma ; ii) wapiga kura hawadhani kwamba ushuru wanaolipa unastahili kwa wao kudai kiwango fulani cha utendaji, ambayo ina maana kwamba wapiga kura wamekubali utendakazi usioridhisha kutoka kwa wale waliowachagua. Hii inapaswa kuwa sababu ya kushtusha; zaidi ya hivyo, wakati mtu anapouliza swali “Kama si matarajio ya ubora na utoaji wa huduma kwa wakati, na utendaji kazi wa viongozi waliochaguliwa au kwa wapiga kura kupata thamani ya fedha zao (Kodi) , inayowafanya Wakenya kupiga kura katika uchaguzi mkuu, je nini?” Kwa hakika hii ni sehemu inayohitaji masomo zaidi. Nini hasa mamlaka, majukumu, wajibu au kazi ya wabunge (MPs) na maafisa wa serikali waliochaguliwa kuhudumu ili wapate malipo na faida wanazopata, na hata kufikiri wao wanahitaji zaidi? Muhtasari huu unatoa maelezo mafupi ya majukumu mbalimbali ya maafisa wa serikali waliochaguliwa wanapaswa kufanya. Muhtasari huu umetengezwa kukabiliana na masomo5 ambayo yalibainisha haja ya kujenga uwezo wa wabunge kuelewa na kutekeleza bora majukumu yao. Muhtasari huu pia unatambua haki ya na wajibu wa ushiriki wa raia ambao sasa unatambuliwa katika Katiba ya Kenya, 2010.
DOWNLOAD
cross
linkedin facebook pinterest youtube rss twitter instagram facebook-blank rss-blank linkedin-blank pinterest youtube twitter instagram